Swahili
Surah Al-Qadr ( The Night of Decree ) - Aya count 5
Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu.
Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri?
Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.
Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo.
Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.